Mkali wa hip hop, Bongo Nay wa Mitego amezidi kumrushia maneno ya kejeli rapa mwenzake, Godzilla ambaye kwasasa ameshuka kimuziki.

Nay wa Mitego kupitia mtandao wa Instagram ameandika maneno ya kumuudhi mkali huyo kutoka pande za Salasala kuhusu kushuka kwake kimuziki huku akisema kuwa nafasi yake imezibwa na Billnass.

Kupitia akaunti yake Instagram Nay ameandika “Ujinga Ni Kukasilika Pale unapo Ambiwa Ukweli. Una panic #MotoWatag Walio Panic na Kubishana na Ukweli mi naanza na @kingzilla_tz  aiseh Yule Mwanamke nitakupa Number yake Mi Mwenyewe Japo Najua huto Muweza. Ila @billnass Una Roho Mbaya sana Kijana Hutaki Kumpa ata Upenyo Kaka ako.!?, Njo Nikusaidie @kingzilla_tz Maana Stress Ulizo nazo Utaja kula Ngada Bureeeee. Karibu #FreeNation966 Tuta kurudisha kwenye Game.!, #Moto

Nay wa Mitego ni rapa ambaye amezoea kuingia kwenye bifu na wasanii wenzake ambapo anawaimba kwenye nyimbo zake pamona na kuwakejeli kupitia mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *