Aliyekuwa waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema kuwa atazungumza na waandishi wa habari kuhusu suala la kutenguliwa na Rais Magufuli.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amebadilisha Baraza la mawaziri na kutemtengua aliyekuwa Waziri wa Waziri wa Habari , Utamaduni , Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na nafasi yake kuchukuliwa na Dkt. Harrison Mwakyembe.

Nape alikuwa mstari wa mbele kufuatila tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kuvamia kituo cha Clouds FM.

Kupitia akaunti yake ya Twitter Nape amesema kuwa baadaye atazungumza na waandishi wa habari kuhusu kipigwa kwake chini.

Ujumbe wake ameandika kama ifuatatvyo “Ndugu zangu naomba TUTULIE! LEO mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba TUTULIE,” alitweet Waziri Nape.