Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo amefunguka na kuwatia moyo vijana waache tabia ya kuishi katika maisha ya kulia kila siku bali wanapaswa waishi kwa furaha ili waweze kupata baraka za Mungu.

Mrisho Gambo amesema kupitia ukurasa wake maalum wa Facebook baada ya kuwepo na desturi ya watu wengi kuwa na uoga wa maisha huku wengine wakiogopa kusema mbele za watu kwamba huwa wanalia kutokana na kukosa jambo fulani katika maisha yao.

“Usiishi maisha ya kulia kila siku, lazima ifike kipindi useme sasa kulia basi. Kulia kwa uchungu sio maisha, maisha ni kulia kwa furaha, wengi wanaona aibu kusema wamelia sana, mimi nitakuambia ukweli ninalia sana lakini ninamlilia Mungu simlilii binadamu”,.

Pamoja na hayo, Mrisho ameendelea kwa kusema “Anza kulia na Mungu wako, wanaokucheka waache uchungu ni wao, lia kwa ajili ya watoto wako. Mlilie Mungu kwa ajili ya wazazi, kazi na biashara yako, Mungu akikufuta machozi utaona baraka hata kwa watoto wako, wazazi, kazi hata biashara yako”,.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *