Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amewapa pole watani wake klabu ya Yanga kufuatia taarifa ya jengo la Yanga kupigwa mnada Jumamosi ya wiki hii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Haji Manara ameandika maneno ya kuwapa pole wata zake hao Yanga huku akiweka picha ya jengo la klabu hiyo yenye makao makuu yake mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaa.

Manara ameandika kuwa “Mungu wangu,Jumosi hii jengo la Yanga linapigwa mnada, Wizara ya Ardhi waoneeni huruma kidogo wenzetu wana Swaumu kali, Daah!!sasa watahamia wapi? Shubamit”

Jengo la klabu ya Yanga jijini Dar es Salaam linatarajiwa kupigwa mnada Agosti 19 kwa amri ya Mahakama baada ya kudaiwa kodi ya ardhi zaidi ya milioni 300.

Simba na Yanga zinatarajiwa kucheza mechi ya  ngao ya jamii katika uwanja wa Taifa siku ya Jumatano ya tarehe 23 Agosti 2017.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *