Jakate Mwegelo amekutana na kusalimiana na wanamuziki nyota wa Marekani, Jay Z na Beyonce kwenye mechi ya NBA All-Star Game iliyofanyiak jana katika uwanja wa Smoothie King Center jijini New Orleans.

Jakate a.k.a Kidoti kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti picha akiwa na wakali hao ambao ni wanandoa wenye mtoto moja na wanaoatarajia watoto mapacha hivi karibuni huku akiandika maneno mazuri juu ya kukutana na wanamuziki hao.

Kupitia kaunti yake ya Instagram Jokate ameandika  “So NBA Africa took me courtside and I haaaaaaad to say hello to the Carters,”.

“OMG . @beyonce is super cute and I can’t believe she shook my hand and was like nice to meet you. . I was like wait I need a picture, I came all the way from Tanzania for this B . She’s so sweeeeeet and I’m so lucky lmao,” ameongeza.

“Thank you @beylite @balleralert for this pic I couldn’t snap one as I was shocked and still in disbelief.  #Beyonce #Beylite #NBAAfricaGame #NBAAllStar #Kidoti .”

Kidoti yupo nchini Marekani kwa safari zake za kikazi nchini humo ambapo amepata fursa ya kukutana na mastaa kibao nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *