Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Jerry Muro amemaliza kutumikia adhabu yake baada ya kufungiwa na shirikisho la soka nchini TFF.

Jerry alifungiwa mwaka jana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TTF) kwa mwaka mzima kutojihusisha na shughuli zozote za kimichezo kutoka na utovu wa nidhamu.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instagram hiyo Jerry aliandika maneno kuhusu mwisho wa adhabu hiyo.

Jerry Muro ameandika Natabasamu kwa kuwa Leo 02/07/2017, nimemaliza kutumikia Adhabu “DHALIMU” Kikombe nilichonywea mimi na wao wamekipokea wanaanza kunywea humo, Maisha ni kama Gwaride Kiongozi akisema Nyumaa Geuka wa mbele anakuwa wa MWISHO na wa mwisho anakuwa wa KWANZA, Vumilia ndugu YANGU @hajismanara nakuaubiria “USWAHILINI” Kaeni tayari kwa ujio Mpya @yangasc@simbasc @azamfc

Msemaji huyo alikaa mwaka mmoja nje ya soka kutokana na kifungo hiko kutoka shirikisho la soka nchini TFF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *