Baada ya malalamiko ya Petit Man Wakuache Kuhusu Kunyimwa Kumuona Mtoto wake, aliyekuwa mke wake Esma Platnumz amefunguka kuhusu suala hilo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameanza kwa kuandika “Hii picha nimepiga Nyumbani kwa Naseeb baada ya kufukuzwa na mwanaume niliyezaa nae na kunitupia vitu vyangu nje aliambiwa achague kati ya mimi au mtu aliyekuwa nae kipindi hicho alimchagua huyo mtu na Kwenye kipindi juu alienda kunikashifu na Talaka juu Mtoto alikuwa anamiezi 3”.

Esma Platnumz, “Nakumbuka hapa nilikuwa sina hata mia sina maziwa pampers wala nini mwanaume unampigia sim kuhitaji vitu vya mtoto anakuwekea loudspeaker wanakucheka na watu wake au laah akuchezee anavyotaka then akupe hela ukiondoka nyuma unakutana na matusi kakutukana kwenye mitandao nilipiga moyo konde nikachoka nikajiamulia kujiuzia vimafuta na kuachana nae kabisa nakumbuka nilianza na machupa matano ya mafuta na nilikaa mwezi mzima mpk kupata wateja ila namshukuru Mungu”.

Esma Platnumz, “Wengi humu humu mtandaoni walinicheka na kunitukana na kuhisi nimechanganyikiwa, Now mfanyabiashara nauwezo nikalipia watoto wangu Feza, East African, Tulikuwa tunarudiana na wanaume huenda atabadilika akajua majukumu yake, Mwanamke unayenichamba mimi wewe ungeweza!!?… Hadithi fupi tuu nimekutolea na kutangaza hajazaa na mimi bali amezaa na mdogo wangu”.

Esma Platnumz, “Kumbuka unavyonisapoti mimi kuja dukani kununua vitu unanisaidia watoto wangu waende shule na wale, Tusikubali kijana wa mjini kwa mjini wake akutishie maisha mwanamke simama imara usikubali kudharaulika, Naongea km mama mwenye uchungu Sipendelei kuongelea nina vingi mno ila kukaa kimya kunachosha niacheni na Amani yangu na watoto wangu tabu nilizozipata Mungu na Malaika wake ndo anajua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *