Alichoandika Diamond kuhusu kuwasaidia wasanii

0
69

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefunguka na kusema kuwa anakatishwa na tamaa ya kusaidia wasanii kutokana na wanachomfanyia baada ya kutoka.

Kupita kwenye comment aliyoiandika katika ujumbe uliochapishwa na kaka yake Romy Jons akimashauri kupambana na muziki wake zaidi kuliko kusaidia wasanii ambao baadaye wanaanza kumsema vibaya pembeni na kumkebehi, Diamond ameandika;

“Hivi saa ndio nimegundua kwanini watu kama kina Kidayo, Davido na kadharika waliamua kufocus na nafasi zao na sio kupoteza nguvu, umaarufu, pesa na muda wao kusaidia wasanii chipukizi walowa-sign.

“Hii industry haina shukrani! But usiumie hii ni nchi yetu na ni jukumu letu kuhakikisha kwamba tunaendelea kunyanyua vijana toka mtaani ili nao wajikomboe kimaisha,” amesema Diamond.

Kauli hii inakuja ikiwa ni takribani miezi miwili tangu aliyekuwa msanii wake, Rayvanny kuondoka katika lebo hiyo huku wasanii hao wakifikishana Basata ili kufikia maafikiano ya kumalizana kwa amani.

LEAVE A REPLY