Baada ya Rayvanny kushinda tuzo ya BET katika kipengele cha ‘Viewers Choice Best New International Act Artist’ Diamond amuandikia ujumbe mzito kwa ushindi huo.

Diamond amesema kuwa zaidi ya miaka mitatu tunaenda na kurudi patupu lakini safari hii si patupu tena kufuatia ushindi wa mwanamuziki huyo kutoka lebo ya WCB.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Diamond ameandika “Hatimaye leo Unakuja nayo Tanzania Dah! ….Zaidi ya miaka mi 3 tunaenda na kurudi Patupu….Hakika Maisha Uvumilivu na kutokata tamaa…. BRING IT HOME BOSS!!! @babutale”

Pia ameendelea kuandika “WOOOOOOOOOYOOOOOOOO!!!!!!!….. Nikishindwa kwa Mkono wa Kulia, ntatumia hata Mkono wa Kushoto…..ila lazma ifike @Wcb_Wasafi TANZANIA!!!! Chkua hiyo #Wcb_Wasafi #WinningTeam!”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *