Baada ya Serikali ya Kenya kusitisha uingizaji wa gesi kutoka Tanzania, mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amesema kuwa ni vizuri nchi hiyo ikaheshimu mikataba ya ‘East African Community (EAC)’.

 Bashe amesema hayo baada ya serikali ya Kenya kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Andrew Kamau kupiga marufuku uagizaji wa gesi ya kupikia kutoka Tanzania kupitia mipaka ya nchi hiyo.

Kupitia akaunti yake Twitter Bashe ameandika “Serikali ya Kenya imezuia gesi za matumizi ya nyumbani zinazotoka Tanzania kuingia Kenya ni vizuri Kenya ikaheshimu ‘EAC treaty common’……Dar es salaam ‘port and Cost’ ya gesi inayotoka Tanzania ndiyo ‘competetive edge’ ya makampuni ya Tanzania dhidi ya yale ya Kenya uamuzi huu si sawa”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *