Mkongwe wa muziki wa Marekani, Akon huenda akaingia deal na staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba.

Uwezekano huo unatokana na KING kuingizwa kwenye orodha ya mastaa chipukizi watakaotumbuiza kwenye tamasha lililoandaliwa na Akon liitwalo PASSPORT EXPERIENCE.

Ali KING Kiba kabla ya kukutana na Akon ataanza kuonyesha uwezo kwenye tamasha la SXSW litakalofanyika baadae leo nchini Marekani kwenye jimbo la Texas.

Kiba anatarajiwa kuonyeshana uwezo na mastaa wengine wa kimataifa akiwemo mkali wa Nigeria May D, staa wa Uholanzi DJ WaxFiend na mastaa wa Jamaica Charly Black na Ayo Jay.

Kwenye orodha hiyo, Kiba anaungana na mastaa wa Jamaica, Ayo Jay na Charly Black pamoja na msanii wa Nigeria, May D.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *