Mastaa wa Bongo fleva, Ali kiba na Mr Blue wanatarajiwa kumrudisha Abby Sklillz kwenye anga ya muziki wa Bongo fleva baada ya  kushirikishwa na msanii huyo kwenye nyimbo mpya itakayotoka hivi karibuni.

Mastaa hao ni miongoni mwa wasanii wanofanya vizuri katika anga ya Bongo fleva huku Ali Kiba akitamba na nyimbo “Aje” na Mr Brue akitamba na nyimbo ‘Mboga Saba” wameshirikishwa kwenye nyimbo hiyo ili kumsapoti Abby Skillz ambaye kwasasa kashuka kimuziki.

abby

Baadhi ya kipande ambacho ameimba Ali kiba kwenye wimbo huo kimepokelewa vizuri na mashabiki ikiwa ni ishara kwamba wimbo huo utafanya vizuri na kumrudisha kwenye ramani ya muziki msanii Abby Skilliz ambaye kwa muda mrefu alipotea kwenye soko la muziki.

Si mara ya kwanza kwa wasanii hao watatu kukutana kwenye nyimbo moja kwani walishafanya ivyo miaka ya nyuma baada ya Abby Skillz kuwashirikisha Ali Kiba na Mr Brue kwenye nyimbo iliyokuwa inaitwa “Maria” ambayo ilipata umaarufu sana kwa mashabiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *