Mwanamuziki nyota wa Bongo fleva, Alikiba anatarajiwa kutumbuiza kwenye utoaji wa tuzo za MTV MAMA zitakazofanyika katika jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini Oktoba 22 mwaka huu.

Meneja wa msanii huyo, Seven Mosha kupitia ukurasa wake Instagram ameweka picha ya Alikiba na kuandika ujumbe unaosomeka, “The King @officialalikiba is set to perform at the MTVAfrica Music Awards 2016 .”

Kwa upande wa MTV Base nao wameandika: Yes,@OfficialAliKiba to bring that HEAT to the stage.

Alikiba ataungana na wasanii wengine kutumbuiza kwenye tuzo hizo ambao ni Yemi Alade, Nasty C, Babes Wodumo na wengine wengi.

 Kwa mwaka huu tuzo hizo zina vipengele 18 ambavyo wasanii kutoka nchi mbalimbali za Afrika watawania.

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Ticketpro Dome jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini Jumamosi ya Oktoba 22, mwaka huu.

Alikiba ni miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri barani Afrika kwasasa kutokana na vibao vyake kugusa nyoyo za mashabiki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *