Ali Juma Ali ameptishwa na CCM kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge, Jimbo la Dimani katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Januari 22 mwakani.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Vuai Ali Vuai alisema Kamati Maalumu baada ya kupitia majina ya wagombea 25 yaliyowasilishwa, jina la Ali Juma Ali ndiyo lililopendekezwa kugombea nafasi hiyo katika kinyang’anyiro cha uchaguzi huo mdogo wa Dimani.

Vuai meisema kikao hicho kilifanya baada ya chama kupokea majina ya wanachama hao 25 waliojitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi.

Aidha kamati maalumu imewataka wanachama wa CCM kushiriki kikamilifu katika harakati za kampeni za uchaguzi mdogo na kuhakikisha kwamba chama hicho kinashinda katika uchaguzi huo.

Uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani unafanyika kufutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wake, Hafidh Ali Tahir (CCM) kilichotokea Novemba 11 mkoani Dodoma alikokuwa akihudhuria Mkutano wa Bunge na kuugua ghafla.

Mgombea huyo wa nafasi ya ubunge kwa tiketi ya CCM anatarajiwa kuchuana na mgombea atakayepitishwa na Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kimetangaza kushiriki katika uchaguzi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *