Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa kiungo, Alex Oxlade-Chamberlain kutoka Arsena kwa dau la paundi milioni 40.

Mchezaji huyo amejiunga na Majogoo hao wa Anfield kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 40.

Awali Chamberlain alikuwa akiwaniwa kwa ukaribu na Chelsea ambayo hakufanikiwa kuipata saini yake.

Mchezaji huyo amewashangaza mashabiki wengi baada ya kukataa kuongeza mkataba mpya na Arsenal ambao ungemfanya kuweza kulipwa kiasi cha paundi 180,000 kwa wiki na badala yake amekubali kujiunga na Liverpool kwa kulipwa mshahara wa paundi 120,000 kwa wiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *