Watu 15 wameuawa na wengine wamejeruhiwa katika mashambulio ya mabomu ya anga katika mji wa Aleppo nchini Syria.

Afisa wa Uangalizi wa masuala ya haki za binadamu nchini Syria mwenye makao yake nchini Uingereza amesema kuwa ndege za utawala wa Syria zilirusha vilipuzi viwili vilivyosheheni makombora yaliyotengenezwa ndani ya mapipa kwa dakika kadhaa tofauti ambayo yaliangukia karibu na hema ambako jamaa wa watu waliouawa kwa mabomu wiki iliyopita walipokuwa wakipokea rambi mbali.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema bomu la kwanza liliuvutia umati wa watu kukimbilia eneo la tukio ambako bomu jingine lilipiga na kuwauwa watu zaidi na kuharibu gari la kubebea wagonjwa.

Inaaminiwa kuwa makumi kadhaa ya watu wamejeruhiwa na idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *