Kundi la waasi nchini Syria limesema litakutana na maafisa wa Urusi na wale wa Uturuki kuzungumzia swala la kusitishwa kwa mapigano huko Syria.

Kundi hilo Ahrar al-Sham limesema tayari limefanya mazungumzo na Uturuki lakini bado mwafaka haujapatikana kwasababu ya kutojumuishwa kwa eneo moja muhimu lililoko karibu na Damascus kwenye mazungumzo hayo.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu amesema nchi yake imekubaliana na Urusi na vilevile Iran kuwe na ushirikiano wa karibu katika lengo la kutafuta amani ya kudumu huko Syria.

Nchi ya Syria imekumbwa na mapiano kati ya majeshi ya serikali na yale ya waasi ambao wanataka kuundoa utawala wa rais wa sasa wa nchi hiyo Bashar al-Assad anayeungwa mkono na Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *