Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mwanaharakati wa kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi, Babu Sikare maarufu kama Albino Fulani amefariki dunia.

Albino Fulani ambaye amewahi kutamba na nyimbo kadhaa ikiwemo “Nafasi” aliyoshirikiana na Mwana FA, Sugu na Belle 9 amefariki Dunia akiwa Nchini Marekani.

Mwana FA ambaye ni rafiki yake wa karibu amesema chanzo za Kifo cha Albino Fulani ni maradhi ya Saratani ya Ngozi ambayo aliwahi kupona siku za nyuma lakini ikarejea tena na kumsumbua hadi mauti yalipomkuta.

Mwana FA amesema alizungumza na Albino Fulani wiki kadhaa zilizopita ambapo alimpa taarifa kuwa Madaktari wamemwambia ana muda mfupi wa kuishi kutokana na Saratani yake kusambaa sehemu kubwa ya mwili wake na kuathiri Afya yake kiujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *