Mwanamuziki nyota wa Marekani, Rick Ross ametangaza rasmi ujio wa album mpya inayoitwa kwa jina la Rather You Than Me kupitia lebo ya Epic Records.

Album hii itatoka mwaka 2017 na ni album ya kwanza ya rapa huyo baada ya kutoka Def Jam alipofanya album yake ya mwisho ya Black Market iliyoshika namba 6 kwenye chati za Billboard 200 mnamo December 2015.

Rick Ross hivi karibuni ametoa wimbo akiwa na 2 Chainz na Gucci Mane “Buy Back the Block,” ambayo nayo itakuwepo kwenye album ijayo.

Ikumbukwe kuwa mwanamuziki huyo hivi karibuni alipunguza bei ya nyumba yake kutokana na kushuka kiuchumi.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *