Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara amewapandisha vyeo makamanda wa zamani wa kikundi cha waasi ambao walisaidia kuzima vuguvugu la mgomo ambalo lilijitokeza mapema mwezi huu.
Shirika la Associated press limedai kuwa Lt-Col Issiaka Ouattara amepandishwa cheo na sasa atakuwa mkuu wa Republican Guard, wakati ambapo Lt-Col Cherif Ousmane amepangiwa kuongoza kikosi cha usalama wa taifa kutoka kwenye kikosi cha ulinzi wa rais.
Makanda hao wawili walikuwa ni sehemu ya waasi wakati wa mgogoro ulioigawa nchi hiyo inayoongoza kwa uzalishaji wa Cocoa duniani, mwaka 2002 hadi 2011.
Pia makamanda hao walihusika vilivyo katika kufanikisha rais Alassane Ouattara kutwaa madaraka mwaka 2011 baada ya rais wa wakati huo, Laurent Gbagbo.
Makamanda hao wawili ndio waliokuwa sehemu ya wawakilishi wa serikali ambao waliafikiana na waasi wa zamani ambao walianzisha mgomo kwenye miji ya Ivory Coast kwa kutaka malipo ya bonsai ambazo zilikuwa hazijalipwa.