Klabu ya Crystal Palace imemfukuza kazi kocha wake, Alan Pardew baada ya timu hiyo kupata matokeo mabaya hivi karibuni mpaka kupekeleke kushika nafasi ya 17 kwenye msimami wa ligi ya Uingereza.

Kocha huyo alijiunga na klabu hiyo januari 2015 baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu lakini sasa mkataba huo umekatishwa kutokana na matokeo mabovu ya Crystal Palace.

Alan Pardew  mwenye umri wa miaka 55 amefukuzwa kazi baada ya kushinda mechi moja tu kati ya 11.

Palace imejipatia pointi 26 kutoka mechi 36 ilizocheza 2016 na iko pointi moja tu juu ya timu zilizo katika hatari ya kushushwa daraja.

Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Sam Allardyce anapigiwa upatu kuchukua wadhfa huo baada ya kutimuliwa kwa kocha huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *