Jumla ya watu 12 wamefariki na wengine kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kushambulia eneo moja la makazi katika mji wa Mandera kaskazini mashariki mwa Kenya.

Polisi na wanajeshi kwa sasa wanafanya msako na kushika doria mjini katika mji huo kufuatia ukio hilo.

Mji wa Mandera umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa al-Shabaab, kundi linalopigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika taifa jirani la Somalia.

Wanamgambo hao wamekuwa wakishambulia watu ambao si wa asili ya Kisomali wakitaka serikali ya Kenya kuondoa majeshi yake nchini Somalia yanayolinda amani..

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *