Kundi la wapiganaji la Al Shabab wamewachinja raia 9 wa Kenya katika kijiji cha Poromoko siku ya Jumamosi nchini humo.

Polisi wameviambia vyombo vya habari kuwa washambuliaji hao wanahisiwa kuwa wameingia Kenya kupitia mpaka wa Kenya na Somalia.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa nchi yake imepata majanga mawili kwa wakati mmoja kwani  Kenya bado ilikuwa inaomboleza kifo cha waziri Joseph Nkaissery.

Vilevile rais Kenyatta  amewaahidi wananchi kuwa nchi yake itaongeza mbinu za kulinda usalama wa raia wake.

Hata hivyo polisi wameongezwa kulinda zaidi mahala tokeo hilo lilipotokea ili kudhibiti vitendo hivyo visitokee tana nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *