Kundi la wanamgambo la al-Shabab la nchini Somalia limewaua wanaume wanne waliolaumiwa kwa kuipelelezea Marekani, Kenya na serikali ya Somalia inayoungwa mkono na nchi za magharibi.

Wanaume hao walikatwa vichwa hadharani kwenye mji ulio wilaya ya Jamame eneo la Jubba karibu kilomita 70, kaskazini mwa mji wa Kismayo baada ya kupatwa na hatia na mahakama ya Sharia.

Wanaume hao walikiri kuwa walikuwa wapelelezi, kwa mujibu wa gavana wa al-Shabab Abu Abdalla eneo la Jubba.

Kundi hilo limethibitisha kufanya hivyo kutokana na wanaume hao kupatwa na hatia ya upelelezi nchini Somalia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *