Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri imetinga fainali ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kuifunga Etoile du Sahel ya Tunisia.

Mshambuliaji Walid Azarou alifunga mabao matatu (hat-trick) kwenye ushindi wa mabao 6-2 ilioupata Al Ahly.

Mabao mengine ya Al Ahly yalifungwa na Ali Maaloul pamoja na Rami Rabiaa huku Hamdi Naguez wa Etoile du Sahel akifunga na kukamilisha mabao 6 ya Ahly.

Al Ahly imeshinda kwa jumla ya mabao 7-4 na kutinga fainali ambapo sasa itacheza na Wydad Casablanca ya Morocco.

Al Ahly ni mabingwa wa Kihistoria wa ligi ya mabingwa Afrika wakiwa wametwaa kombe hilo mara 8 na endapo wataifunga Wydad Casablanca wataongeza rekodi yao.

Wydad Casablanca watakuwa wanatafuta taji la pili la ubingwa wa Afrika ambapo mara ya mwisho walitwaa mwaka 1992 kabla ya kupoteza fainali mwaka 2011 dhidi ya Esperance.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *