Mgombea urais kupitia upinzani nchini Ghana, Nana Akufo-Addo ameshinda uchaguzi wa urais nchini humo kwa kumuangusha John Mahama.

Nana Akufo-Addo, alishangilia ushindi wake na kusema taifa hilo sasa ni mwenge wa demokrasia Afrika Magharibi.

Ameahidi kukabiliana na uchumi uliozorota, swala ambalo lilitiliwa mkazo wakati wote wa kampeni,

Akufo-Addo alisema kuwa ushindi wake ni hatua anayofurahia sana katika maisha yake yote na akaahidi kuwa atafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa anatekeleza matakwa ya wananchi wa Ghana.

Amepongezwa na mshindani wake mkuu, rais John Mahama, aliyeahidi kuheshimu matokeo ya uchaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *