Mwanamuziki nchini Kenya, Akothee amesema kuna uwezekano akaachana na muziki baada ya kumpata mpenzi mpya ambaye ni ‘Mzungu’.

Inadaiwa kwamba mpenzi huyo wa sasa hataki kusikia masuala ya muziki hivyo amemuomba mrembo huyo kuachana kabisa na muziki na achague kazi nyingine ya kufanya.

Mwanamuziki huyo mwenye watoto watano, aliwahi kusema kuwa katika maisha yake hawezi kusumbuliwa na mwanamume yeyote kwa kuwa anaweza kuendesha maisha yake mwenyewe.

Akothe amesema kuwa “Mzungu wangu yuko moyoni, lakini amenishangaza kuniambia niachane na muziki, hivi inawezekana kweli? Sidhani kama ninaweza kufanya hivyo lakini ninampenda sana na muziki ni sehemu ya maisha yangu hadi nafikia hatua hii,”.

Mwanamuziki huyo amepata umaarufu katika nchi za Afrika Mashariki kutokana na umahiri wake katika uimbaji wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *