Rapa wa Hip Hop nchini Marekani, Akon yupo ziarani nchini Liberia kuweka umeme wa jua katika shule mbili za msingi katika taifa hilo la Afrika Magharibi.
Huo ni miongoni mwa miradi yake ya kuwawekea umeme watu milioni 600 katika bara la Afrika.
Akon ambaye ni mzaliwa wa Senegal anashirikiana na kampuni ya Bridge International Academies pamoja na ushirikiano na mashirika mengine ya kimatifa kusimamia shule 50 nchini Liberia.
Wakati msafara wake wa magari ulipokuwa ukipita katika mji mkuu wa Monrovia,chini ya ulinzi wa maafisa wa polisi mwanamuziki huyo alisema kuwa inasikitisha kuona kwamba hakuna umeme katika barabara ya kilomita 50 kutoka uwanja wa ndege.
Mradi huo wa Akon utasaidia watu wa bara la Afrika kuweza kuwa na umeme tofauti na sasa ambapo changamoto za ukosefu umeme umekuwa mkubwa sana.