Video ya wimbo mkali wa Bongo fleva, Alikiba ‘Aje’ imefanikiwa kushinda tuzo ya video bora ya mwaka kwenye tuzo za Soundcity MVP 2016 zilizofanyika jana katika jiji la lagos nchini Nigeria.

Tuzo hizo zilishuirikisha jumla ya washiriki 109 huku washiriki 14 ndiyo wameibuka na ushindi katika tuzo hizo za muziki nchini Nigeria.

Wasanii waengine walioshinda tuzo hizo ni Sauti Soul kutokea pande za Kenya ambao wameshinda tuzo ya kundi bora la mwaka kwenye tuzo hizo.

Mbali na hayo Mwanamuziki wa Nigeria, Wizkid amefanikiwa kushinda tuzo ya Mwanamuziki bora wa mwaka kutoka Afrika ambayo hiyo ndiyo tuzo kubwa usiku wa jana nchini Nigeria.

Wasanii wengine wa Bongo Fleva walioshiriki tuzo hizo lakini hawakufanikiwa kupata ni Diamond, Vanessa Mdee na Navykenzo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *