Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, mhandisi Hamad Massauni amesema kuwa ajali za barabarani zimepungua kwa asilimia 10 ambapo katika kipindi cha miezi sita vifo vimepungua kwa asilimia 19.

Mhandisi Masauni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa  tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa baraza hilo katika kupunguza ajali za barabani.

Aidha amesema kuwa miongoni mwa malengo makubwa ya tathmini hiyo ni kupunguza ajali, vifo na majeruhi, ukamataji wa makosa ya usalama barabarani  kwa magari na pikipiki, elimu ya usalama barabani kwa watumiaji wa barabara na hata usimamizi wa sheria.

Naibu waziri huyo amefafanua kuwa tathmini ilionyesha kuwa miezi miwili kabla ya mkakati huo makosa mbalimbali ya usalama barabarani yalikuwa ni 324,284 katika miezi miwili na  baada ya mkakati kulikuwa na  makosa 393,728 ambalo ni  ongezeko la makosa 69,444  ambayo ni sawa na asilimia 21.

Pia ameeleza pia kipindi hicho cha miezi miwili kabla ya mkakati kulikuwa majeruhi 135 na miezi miwili baada ya mkakati kulikuwa na  majeruhi 113 na kuonyesha upungufu wa majeruhi 22 ambayo ni sawa na asilimia 16.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *