Watu tisa wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea eneo la Ifunda mkoani Iringa jana baada ya lori kugongana na gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyosababisha vifo na majeruhi mkoani humo.

Masenza amesema dereva wa lori lililopata ajali lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam, alishindwa kufunga breki na kuigonga Hiace iliyokuwa imeegeshwa pembezoni mwa barabara.

Mkuu mkuu wa mkao huyo amesema katika ajali hiyo iliyotokea jana jioni, madereva wa magari hayo wote wamejeruhiwa na wamelazwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa pamoja na majeruhi wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *