Staa wa filamu na mtayarishaji wa Bongo movie, Jacob Stephen ‘JB’ jana amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya ya gari .
JB ambaye hivi karibuni alikuwa mkoani Arusha katika shindano la Mama Shujaa, amewataka mashabiki wake kutambua kwamba anaendelea vizuri pamoja na wanzake ambao walikuwa kwenye gari hilo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram JB ameandika ‘Asanteni wote mlionipa pole kwa ajali ya jana’ . “Hakika Mungu ni Mwema, nipo poa mimi na wenzangu wote. Namshukuru sana Mungu.Thank you JESUS,”.
JB kwasasa anafanya vizuri na filamu yake mpya inayoitwa kwa jina la ‘Kalambati Lobo’ ambayo inafanya vizuri hadi sasa.