Kampuni ya ndege ya Air India imezindua ndege itakayokuwa na viti vya wanawake pekee kwa lengo la kukabiliana na unyanyasaji wa kingono .

Wanawake kadhaa akiwemo muhudumu mmoja wa ndege wamelalamikia ndege hiyo wakidai kuwa wamekuwa wakinyanyaswa kingono na abiria wa kiume.

Viti maalum kwa ajili ya wanawake kwenye ndege ya shirika la ndege la Air India
Viti maalum kwa ajili ya wanawake kwenye ndege ya shirika la ndege la Air India

Mkuu wa muungano wa Abiria nchini humo amepinga mpango huo wa viti, akiutaja kuwa wa kiubaguzi.

Hatua ya kutengeza viti kulingana na jinsia fulani sio jambo la kawaida kimataifa kwani imezoeleka kila ndege inakuwa na viti mchanganyiko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *