Mwanamke mmoja wa jimbo la Oregon nchini Marekani amenusurika baada ya chatu mtoto kuingia kwenye tundu la kuvalia hereni la sikio lake.

Mwanamke huyo, Ashley Glawe amepost picha yake kwenye mtandao wa Facebook akiwa hospitali na kuandika:

‘BY FAR one of my #CRAZIEST life moments! Went to the #EmergencyRoom because my #BallPython #Python #Snake decided to get #STUCK in my #Gauged earlobe!’

Kwa mujibu wa mwanamke huyo, chatu huyo mtoto ni wake na anaitwa Bart na wakati wa tukio alikuwa anacheza nae kabla ya kuteleza na kupita kwenye tobo la sikio na kunasa.

‘Ilitokea kwa haraka sana kiasi ambacho kabla sijajua kilichotokea, tayari nilikuwa nimechelewa’

screen-shot-2017-02-02-at-12-25-52

Madaktari walilazimika kulichoma sindano ya ganzi sikio lake na kisha kulitanua na kufanikiwa kumpitisha chatu huyo bila kulikata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *