Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City, Sergio Aguero amepata ajali ya gari iliyotokea jana akiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege nchini Uholanzi ambako alikuwa amehudhuria tamasha la muziki.

Aguero mwenye umri wa miaka 29 amevunjika mbavu na atakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili na atakosa mchezo dhidi ya Chelsea utakaofanyika kesho.

Picha zilizosambaa katika baadhi ya mitandao kutoka nchini Uholanzi zimeonyesha gari ndogo ambayo Aguero alikuwepo na dereva wake ikiwa imegonga nguzo katikati ya jiji la Amstedam huku ikiripotiwa kuwa hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya kuumia.

Awali aliweka picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ikimuonyesha yeye na msanii kutoka Uholanzi anayefahamika kwa jina la Maluma ambaye ndiye aliyemualika katika tamasha hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *