Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero amefungiwa na chama cha soka cha Uingereza (FA) kutocheza mechi nne baada kumchezea vibaya David Luiz.

Aguero mwenye umri wa miaka 28 alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya beki wa Chelsea, David Luiz kwenye mechi iliyomalizika kwa Chelsea kushinda 3-1 siku ya jumamosi.

Mshambuliaji huyo wa Argentina alikuwa ameadhibiwa tena mwezi Agosti alipopewa kadi nyekundu kwa kumchezea visivyo mchezaji wa West Ham Winston Reid.

Mechi nne anazokosa mshambuliaji huyo dhidi ya Leicester, Watford, Arsenal na Hull kwenye ligi kuu nchini Uingereza.

Kwa upande wa mchezaji mwenzake wa City Fernandinho pia alipewa kadi nyekundu uwanjani baada ya kumkaba koo Cesc Fabregas naye amefungiwa kutocheza mechi tatu za ligi kuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *