Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kufanyia kazi ombi la wananchi la kujengewa kituo cha daladala eneo la Daraja la Nyerere.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo jana alipofanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Feri jijini Dar es sa laam na kuvuka bahari kwa kutumia cha MV Kigamboni ambapo pia amekutana na wananchi wa Kigamboni.

Hata hivyo Rais Magufuli baada ya kutembelea daraja la Nyerere na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo ndio akatoa agizo hilo kwa Mkuu wa Mkoa huyo kulifanyia kazi ombi la wananchi kuwajenga kituo cha hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *