Rais wa Zimbambwe, Robert Mugabe amelekwa nchini Singapore kufanya vipimo vya Afya yake kutokana na hali yake kutokuwa sawa.

Mugabe ambaye hivi karibuni amefanya sherehe ya kutimiza umri wa miaka 93 hali imeoneka kutokuwa sawa kutokana na umri wake kuwa mubwa mpaka kupelekea kuandamwa na magonjwa.

Mugabe amekua dhaifu zaidi, na sasa anapata shida hata kutembea wakati wa matukio mbalimbali ya kitaifa.

Msemaji wa rais huyo amesema kuwa vipimo hivyo ni vya mara kwa mara na Rais anatarajiwa kurejea nchini Zimbabwe wiki ijayo.

Mugabe ni kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi duniani, aliingia madarakani mnamo mwaka 1980.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *