Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Chid Benz amesema kuwa licha ya matumizi ya dawa za kulevya kumrudisha nyuma kimuziki, ameahidi kupambana hadi mwisho ili awe balozi bora kwa wasanii wenzake.

Chid Benz ambaye kwa sasa yupo chini ya kituo kinachopambana na matumizi ya dawa za kulevya, amesema anashukuru Mungu anaendelea vyema na ni matumaini yake atarejea katika sanaa yake na kufanya vizuri kama zamani.

Amesema kwa sasa anaona afya yake inazidi kuimarika na Watanzania wategemee mambo mazuri zaidi kutoka kwake, kwani anajiona ana mafanikio makubwa zaidi tangu aachane na matumizi ya dawa hizo.

Chid amesema kuwa anamshukuru Mungu kuona afya yake inazidi kuimarika hasa baada ya upasuaji wake kwenda vizuri.

Pia ameshukuru kuona anazidi kupata sapoti kutoka kwa wasanii na watu wake wa karibu na kujiona katika hatua nyingine ya maendeleo na Watanzania wategemee mambo mazuri kutoka kwake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *