Mastaa wa Bongo fleva, Ali Kiba, Diamond Platnum, Vanesa Mdee na Linah wamechaguliwa kuwania tuzo za Afican Music Magazine Awards “AFRIMMA” zitakazo fanyika nchini Marekani Oktoba 15 mwaka huu.

Diamond Platnum ameongoza kwenye orodha hiyo baada ya kuchaguliwa kuwania tuzo hizo katika vipengele vinne vya msanii bora wa kiume kutoka Afrika Mashariki, nyimbo bora ya kushirikiana, nyimbo bora ya mwaka na msanii bora wa mwaka.

Kwa upande mwingine Ali Kiba amechaguliwa kuwania tuzo ya msanii bora wa kiume kutoka Afrika Mashariki huku Vanesa mdee akiwa kwenye kipengele cha msanii bora wa kike ambapo na Linah yupo kwenye kipengele hiko.

Mastaa wengine kutoka lebo ya WCB, Hamornize yupo kwenye kipengele cha msanii bora chipukizi, huku Moses Iyobo akichaguliwa kuwania tuzo kwenye kipengele cha Dansa bora wa Afrika huku Tuddy Thomas akichaguliwa kuwania kipengele cha mtayarishaji bora wa muziki wa mwaka kutoka Afrika.

Kundi la Yamoto Band ambalo lipo chini ya mkubwa Fella limechaguliwa kuwania tuzo ya kundi bora la Afrika.

Tuzo za ‘AFRIMMA’ ni tuzo ambazo zimejizolea umaarufu mkubwa Barani Afrika na ufanyika kila mwaka nchini Marekani ambapo ujumuisha wasanii mbali mbali kutoka Afrika kuwaniwa tuzo hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *