Aliyekuwa mwanamuziki nyota wa reggae nchini Afrika Kusini, Lucky Dube leo amefikisha miaka tisa toka auawe kwa kupigwa na risasi.

Kwa heshima ya mwanamuziki huyo, waziri wa sanaa na utamaduni nchini Afrika Kusini Nathi Mthethwa amelitaka taifa hilo likumbuke mchango wake kwenye muziki pamoja na jamii kwa ujumla.

Lucky Dube aliuawa siku kama leo Oktoba 18 mwaka 2007 katika kitongoji cha Rosettenville jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini muda mfupi baada ya kuwashusha watoto wake wawili kati ya saba kwenye nyumba ya mjomba wao.

Baada ya tukio la kuawa kwa Luck Dube polisi wamesema watu waliomuua hawakujua kama nini yeye na walidhani ni Mnaijeria.

Watuhumiwa wote waliofanya tukio hilo waliuhukumiwa kifungo cha maisha jela mnamo March 31 mwaka 2009.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *