Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameingia kwenye kashfa mpya baada ya kugundulika mpango wake wa kuhamia nchini Dubai atakapoachia ngazi ndani ya taifa hilo.

Mpango huo umekuja baada ya Rais huyo kuchokwa na baadhi ya wanachama wa ANC nchini humo ambao wamechosha na uongozi wa Rais huyo.

Kwa mujibu wa barua pepe zilizosambaa nchini humo zinasema kuwa rais huyo ana mpango wa kuachia ngazi na kukimbilia nchini Dubai kwa makazi mapya.

Barua pepe hizo zimechapishwa na gazeti moja nchini Afrika kusini na zinaonyesha uhusiano mkubwa kati ya rais wa Afrika kuisni Jacob Zuma na familia yenye utata, Gupta, hususan kuhusu madai kwamba rais Zuma anazingatia kuhamia Dubai.

Wakati chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kinakumbwa na vita vya ndani kwa ndani, barua pepe hizo zinatarajiwa kuibua mjadala mkali kwani zinafichua mipango ya rais Zuma ya kuhamia Dubai.

Barua pepe hizo baina ya mwanawe Zuma, Duduzane, na vigogo wa kampuni inayomilikiwa na familia tatanishi ya Gupta, zinashirikisha barua moja iliyotumwa kwa familia ya kifalme nchini Dubai, ambapo Zuma anasema angetaka kuwa na makao ya pili huko Dubai.

Madai hayo yanaibua mjadala wa iwapo rais Zuma anajiandaa kubwaga manyanga kwani chama cha ANC kinaonekana kumgeuka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *