Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeidhinisha uamuzi wa kulipatia bara la Afrika nafasi tisa timu zinazoshiriki fainali za Kombe la Dunia zitakapoongezwa na kuwa 48 mwaka 2026.
Bara la Afrika kwa sasa huwa na nafasi tano pekee lakini sasa imepanda mpaka kufikia timu 16.
Taifa la kumi kutoka Afrika litashiriki katika michuano ya muondoano ya kufuzu, itakayoshirikisha nchi sita, kuamua atakayefaidi kutokana na nafasi mbili za ziada.
Baraza la Fifa lilitangaza pendekezo lake la kwanza kuhusu mpango wa kugawa nafasi hizo 48.
Afrika – 9 kutoka timu za awali 5
Asia – 8 kutoka timu 4 za awali
Ulaya – 16 kutoka timu 13 za awali
Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean – 6 kutoka timu 4 za awali
Bara la Oceania – 1 kutoka timu 1 ya awali
Amerika ya Kaskazini – 6 kutoka timu 4 za awali