Michuano ya 31 ya kombe la mataifa ya Afrika (Afcon) yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia kesho jumamosi kwa mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Gabon atakapocheza dhidi ya Guiene-Bissau.

Miaka 60 imepita toka michuano hiyo ianzishwe kwa mara ya kwanza mwaka 1957 nchini Sudan huku Misri ikiwa ndiyo nchi pekee iliyotwaa kombe hilo kwa vipindi vitatu mfululizo baada ya kufanya hivyo mwaka 2006, 2008 na 2010.

Mechi 32 zitachezwa katika siku 23 kwa timu 16 ambapo zimegawanyika katika makundi manne na fainali yake itafanyika Februari 5 mwaka huu huku bingwa akiondoka na kombe pamoja na kiasi cha fedha dolla milioni 4 za Marekani.

Michano hiyo ndiyo michuano mikubwa kwa ngazi ya taifa katika bara la Afrika kutokana na kukutanisha miamba ya soka katika bara hilo.

Bingwa mtetezi wa michano hiyo ni Ivory Coast aliyeshinda taji hilo mwaka 2015 baada ya kumfunga Ghana kwenye hatua ya fainali kwa mikwaju ya penati.

Timu ambazo zinapewa nafasi kubwa ya kushinda kombe hilo ni Senegal, Ivory Coast na Misri kutoka na ubora wa vikosi vyao kwasasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *