Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane ‘kwa bahati mbaya’ amewapa tiketi wapinzani wake Cameroon kwaajili ya kucheza mchezo wa nusu fainali ya AFCON 2017 baada ya kukosa mkwaju wa penati.

Pambano hilo baina ya miamba hiyo ya soka la Afrika lilimalizika kwa suluhu ya 0-0 baada ya dakika 120.

Mane, ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi barani Afrika baada ya kukamilisha usajili kutoka klabu ya Southampton na kuhamia kwa miamba ya soka Ulaya, Liverpool alikosa penati iliyookolewa na golikipa wa Cameroon Fabrice Ondoa, kabla ya Vincent Aboubakar wa Cameroon kufunga penati ya mwisho na kuipa Cameroon ushindi wa 5-4.

senegal-mane-missed-a-penalty-afcon-2017

Ingawa wengi waliipa nafasi Senegal ya kushinda mechi hiyo kutokana na ubora wa kikosi chake na matokeo yasiyoridhisha ya Cameroon lakini hali imekuwa kinyume chake.

Cameroon ambao ni mabingwa mara nne wa michuano hiyo, watakutana na Ghana au Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *