Staa mkongwe wa Bongo Fleva, Suleiman Msindi maarufu kama ‘Afande Sele’ amesema bado anamkumbuka mzazi mwenzake mama Tunda ambaye ametimiza miaka 4 tangu alipofariki Agosti 16 mwaka 2013.

Afande Sele ambaye ni baba wa watoto wawili, Tunda na Sanaa amesema kuwa kumbukumbu za mama Tunda huja zaidi anapowaona watoto wao.

Msanii huyo amesema kuwa bado hajapata mtu sahihi ambaye anaweza kuwalea watoto wake kama ambavyo walikuwa wakilelewa na mzazi wao lakini anaendelea kumtafuta.

Afande amesema kuwa ‘’Bado sijampata mwanamke wakumuowa kwakuwa nahitaji mwanamke ambaye atawalea watoto kama ambavyo walikuwa wanalelewa na mama yao,”.

Afande Sele anaendelea kushikilia heshima ya kuwa Mfalme wa Mashairi ingawa kwa kipindi kirefu hajafanya kufanya nyimbo ya aina yoyote.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *