Baada ya klabu ya Simba kuonesha nia ya kutaka kuwasajili wachezaji Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi, Afande sele amewachana viongozi wa klabu hiyo.

Aafnde Sele ambaye ni shabiki wa Simba ameoneshwa kutofuraishwa na viongozi wa klabu hiyo katika usajili wa wachezaji hao.

Kupitia akaunti yake ya Facebook afande Sele amesema kuwa kuwasajili wachezaji hao ni kucheza pata potea huku akisema kuwa haamini kama Tanzania nzima hakuna vijana wenye umri mdogo mpaka kuanza kugombea wachezaji wazee.

Afande amefunguka hayo baada ya mvutano wa vilabu vya mpira nchini kumgombea wachezaji wa kimataifa akiwamo raia wa Rwanda Nahodha Haruna Niyonzima, kabla klabu yake kuthibitisha kushindwana katika maslahi.

“Soka ni mchezo wa umri siamini kama bongo yote hakuna madogo wenye vipaji na nguvu za kuwashinda hawa vibabu tunaolazimishwa kuamini bado wapo kwenye viwango, soka la bongo ni sawa na soka la hongo, uozo na mizozo ndiyo nguzo na gumzo”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *