Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Afande Sele amesema kuwa kwasasa ana imani na kinachofanywa na uongozi wa Rais Magufuli.

Afande Sele amesema moja ya sababu ambayo ilimfanya aingie kwenye siasa ni mambo yasiyofaa yaliyokuwa yakifanywa na serikali za awamu zilizopita, huku akiamini anaweza akaleta mabadiliko, lakini kwa sasa haina haja ya yeye kuendelea kufanya hivyo, kwani uongozi uliyopo upo makini.

Pia amesema kuwa “Nina amini kabisa mambo mengi ambayo nayatazama kwenye nchi yanavyoendelea sina shaka nayo kabisa kwa sasa. Sababu kubwa iliyonipelekea niingie kwenye siasa ni kutokana na utawala mbovu uliyokuwa katika awamu zilizopita.

Ameongeza kwa kusema kuwa Nchi ilikuwa kama Kambale hakuna mtu ambaye anaweza kukemea jambo baya kwa kuwa kila mmoja alijiona mkubwa , nchi ilikuwa inajiendea hovyo hovyo tu.

Mwisho amemaliza kwa kusema kuwa Ndiyo maana nikaamua kuingia kwenye siasa lakini sasa kidogo uliyopo naona unafanya niliyokuwa nayataka”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *