Mwanamuziki nyota wa Uingereza, Adele ameshinda tuzo ya albamu bora kwenye tuzo za Grammy zilizotolewa jana jijini Los Angeles nchini Marekani.

Adele ameshinda tuzo hiyo kwa ajili ya albamu yake inayokwenda kwa jina la 25 ambayo imefanya vizuri duniani kote.

Wakati akipewa tuzo hiyo Adele amesema kuwa Beyonce ndiye aliyestahili zaidi kutunukiwa tuzo hiyo kutokana na uwezo wake wa uimbaji.

Adele amesema kuwa “Ni heshima kubwa sana kwangu na nashukuru, lakini Beyonce ndiye mwanamuziki bora maishani mwangu”.

Wasanii kadha wakiwemo Frank Ocean na Kanye West, waliamua kususia sherehe za mwaka huu za kutoa tuzo kwa washindi kwa msingi ya ubaguzi.

Ocean hata alikataa kuwasilisha albamu yake maarufu ya Blonde ishindanie tuzo akisema tuzo za Grammy hazionekani kuwakilisha vyema watu wa eneo ambalo nimetoka mimi, na kudunisha watu ambao ninadunisha”.

Miaka miwili iliyopita, West aliondoka kwa hasira jukwaani baada ya Beyonce kukosa kutangazwa mshindi kwa albamu yake kwa jina Beck’s Morning Phase.

Albamu ya Adele ya 25 bila shaka ndiyo iliyouza nakala nyingi zaidi miongoni mwa zilizokuwa zinashindania tuzo hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *