Mkali wa muziki kutoka pande za Uingereza, Adele Adkins amesema kuwa anatarajia kufunga ndoa huku akiwataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kuisubiri ndoa hiyo mapema mwaka huu.

Mwanamuziki huyo anayetamba na wimbo wake ‘Hello’ amevishwa pete tangu Oktoba mwaka jana na mpenzi wake Simon Konecki ambaye ameishi naye kwa miaka mitano  na kwasasa wamepanga kufunga ndoa mwaka huu.

Wawili hao walitoa tangazo mwishoni mwa mwaka jana kwamba wanatarajia kufunga ndoa Januari mwaka huu, lakini wamedai tangazo hilo limewekwa kwa muda mfupi, hivyo wamesitisha kufanyika Januari lakini wamedai itakuwa mapema mwaka huu.

Adele akiwa na mpenzi wake, Simon Konecki
Adele akiwa na mpenzi wake, Simon Konecki

Kupitia akaunti yake katika mtandao wa kijamii Adele ameandika “Ni mwaka ambao tulikuwa tunausubiri kwa upande wangu na Konecki, tulikuwa na lengo la kufunga ndoa Januari mwaka huu, lakini tunasogeza mbele kidogo ila itakuwa mapema mwaka huu, watu wakae tayari kwa sherehe hiyo,”.

Mwanamuziki huyo wa Uingereza amejizolea umaarufu kupitia nyimbo zake kufanya vizuri katika mataifa mbali mbali duniani baada ya kibao chake cha Hello kuwa nyimbo bora zaidi kufanya duniani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *